UTAJIRI KATIKA MIRADI YA KUFUGA KUKU
Mradi wa kufuga kuku ni mradi ambao huleta faida kwa muda mfupi sana.
Ili upate faida kubwa ni vizuri ukawa na mradi ambao unaweza kuumudu kwa kuwa na mahitaji muhimu katika mradi wako.
MFANO, mtu anayetaka kufuga kuku tuseme 500 anatakiwa kuwa na vifaranga 550. Awe ana uwezo wa kuwalisha hao vifaranga na kuwapa tiba. Pia awe na uwezo wa kujenga banda bora.
Baada ya hapo kinachotakiwa ni umakini wa kufuatilia mradi katika kipengele cha utoaji huduma kwa kuku hao. Katika kundi hilo la kuku 500, 50 wanatakiwa kuwa majogoo na 450 mitetea.
Katika hao mitetea 450 aslimia 75 wanatakiwa watage kila siku. Asilimia 75 ya 450 ni kuku 337.
Mayai ya kuku hawa huuzwa kwa Tsh. 300@. Hivyo kila siku utapata Tsh 337 x 300 = Tsh. 100000.
Kama mtu anaweza kupata Tsh. 100000 kila siku kwa mwezi una uhakika angalau wa kuweka akiba ya Tsh. 100000 bila shida. Kama utaweka akiba ya fedha hiyo kila mwezi bila shida kwa mwaka utakuwa umeweka akiba ya shilingi milioni kumi na mbili.
Watu wengi wanaweza kufikiri hii ni nadharia ambayo haiwezekani, UKweli ni kuwa hiki kitu kinawezekana bila shida kabisa.
Ikiwa utahitahiji usaidizi njoo kwetu tukuelekeze namna unavyoweza kuondokana na umaskini usio wa lazima.
Kumbukeni ndugu wajasiriamali kwamba ukiamua ni kweli ndoto yako itatimia.
Ili upate faida kubwa ni vizuri ukawa na mradi ambao unaweza kuumudu kwa kuwa na mahitaji muhimu katika mradi wako.
MFANO, mtu anayetaka kufuga kuku tuseme 500 anatakiwa kuwa na vifaranga 550. Awe ana uwezo wa kuwalisha hao vifaranga na kuwapa tiba. Pia awe na uwezo wa kujenga banda bora.
Baada ya hapo kinachotakiwa ni umakini wa kufuatilia mradi katika kipengele cha utoaji huduma kwa kuku hao. Katika kundi hilo la kuku 500, 50 wanatakiwa kuwa majogoo na 450 mitetea.
Katika hao mitetea 450 aslimia 75 wanatakiwa watage kila siku. Asilimia 75 ya 450 ni kuku 337.
Mayai ya kuku hawa huuzwa kwa Tsh. 300@. Hivyo kila siku utapata Tsh 337 x 300 = Tsh. 100000.
Kama mtu anaweza kupata Tsh. 100000 kila siku kwa mwezi una uhakika angalau wa kuweka akiba ya Tsh. 100000 bila shida. Kama utaweka akiba ya fedha hiyo kila mwezi bila shida kwa mwaka utakuwa umeweka akiba ya shilingi milioni kumi na mbili.
Watu wengi wanaweza kufikiri hii ni nadharia ambayo haiwezekani, UKweli ni kuwa hiki kitu kinawezekana bila shida kabisa.
Ikiwa utahitahiji usaidizi njoo kwetu tukuelekeze namna unavyoweza kuondokana na umaskini usio wa lazima.
Kumbukeni ndugu wajasiriamali kwamba ukiamua ni kweli ndoto yako itatimia.
UENDESHAJI WA MRADI WA KUKU
UENDESHAJI WA MRADI WA KUKU WA MAYAI:
Iili
kufanikiwa kufikia malengo ya kufuga kuku wa mayai ni vyema mfugaji
akapata wasaa wa kujiuliza maswali kadhaa ili awe na dira sahihi ya kile
anachotarajia kufanya kutokana na mapato ya mradi huo.
Dira ni picha ya matokeo yanayotarajiwa yanayotokana na juhudi na maarifa .
Bila
shaka kabla ya kuanza kufuga utakuwa umejiuliza ni kwa nini ufuge kuku
wa mayai na wala sio kufanya kitu kingine ; swali kama hili litakusaidia
kuwa na muelekeo wa kile unachotarajia na hivyo kuweka mkakati sahihi
wa kusimamia mradi wako wa kuku wa mayai.Mfano , pengine umeamua kufuga
kuku kwasababu kuna upatikanaji wa pembejeo kwa urahisi kama vile
upatikanaji wa vifaranga, viinilishe, madawa na kubwa zaidi ni
upatikanaji wa soko la mazao yako.
Vyovyote iwavyo mambo yafuatayo ni vizuri yakazingatiwa ili kupata mafanikio katika mradi wa kufuga kuku wa mayai;
1. Uwe na uhakika wa kupata vifaranga kutoka kwa wasambazaji mahiri ( reliable Day old Chicks breeders and Suppliers)
2. Zingatia ratiba ya kulisha. Lisha kuku chakula kinachopendekezwa kwa kuzingatia umri na uzito.
3. kagua
na na fanya usafi mara kwa mara na katika nyakati zilizopangwa(inspect
and carry out specificl and periodical hygienic operations)
4. toa matunzo kwa kwa kuzingatia mahitaji ya makundi.
5. Tengeza
viota ili kuku waweze kutaga mayai kwa faragha bila bughudha kutoka kwa
wengine. Vilevile viota husaidia kuwa na mayai safi na husaidia kuepuka
kuvunja kuvunjika na kuchafuka kwa mayai mara kwa mara.
6. Hakikisha unasafisha mayai kwa kitambaa safi baada ya kuokota na kabla kuwauzia wateja.
7. Zingatia matakwa ya wateja kwa kuainisha mayai katika makundi kama ifuatavyo;
- Rangi ya mayai
- Rangi ya kiini cha yai(egg yolk colour), wengi wanapenda kiini cha rangi ya njano.
- Ukubwa wa mayai
- Aina ya mayai( mayai ya kienyeji yanapendwa zaidi kuliko ya kisasa)
8. Fanya
ukaguzi wa afya za kuku na kuwa tibu kila mara. Utaratibu
unaopendekezwa ni kukagua afya asubuhi unapoamka na usiku unapoenda
kulala. Angalia vinyeo ili kuona wanakunya kinyesi cha rangi
gani(kinyesi ni kielelezo muhimu katika kutambua ugonjwa).
9. Chunguza
tabia za kuku ili kuona kama wanakula mayai au la . Ukiona kuku
wameanza kula mayai fanya zoezi la kukata midomo mara moja kazi hufanywa
na wataalamu , kwahiyo unashauriwa kumuona mtaalmu aliye jirani.
10. Tunza kumbukumbu zote mradi ili zikusaidie kufanya tathmini ya mradi unaoendesha.
KULEA VIFARANGA VYA KUKU
Kulea Vifaranga kwa njia ya asili
Kuku aliyetotoa vifaranga anaweza kuachiwa avilee,
lakini ili kuepuka majanga kama vile vicheche na mwewe inashauriwa
watunzwe ndani ya uzio utakaowazuia ndege hao hatari kuingia na
kuwachukua.
Kulea vifaranga kwa kutumia tetea ni njia ya asili
itumikayo kuatamia, kuangua, kutotoa na hatimaye kuvilea hadi hapo
wanapoanza kujitafutia chakula na kujihami dhidi ya maadui.
Ili kutumia njia hii katika kuangua mayai
kukutolesha mayai na kulea vifaranga ni lazima upate kuku mwenye tabia
ya kuatamia (broody hen).
Kiota cha kuku anayeatamia hutengwa kutoka kwenye
viota vya kutagia. Viota hivi huwekwa matundu mawili ya kuingiza hewa
safi na kutoa ile chafu. Ukubwa wa matundu hayo ni inchi mbili za upana na urefu.
Andaa marandio mapya na kuweka mayai ya kuangua juu
yake; chukua mayai ya kutosha kwenye kiota lakini yasizidi yale
anayoweza kulalia au kuyaatamia (kiasi cha mayai kumi na moja yanatosha
kwa tetea mmoja).
Weka kiota sehemu isiyo na usumbufu kutoka kwa kuku
wengine.kuku wanaofugwa katika kundi ni vizuri ukaweka kwenye uzio kwa
wiki chache ili vifaranga wapate kuota manyoya.
Kuku aliyetotoa karibuni akiwafundisha vifaranga wake wadogo jinsi ya kula.
KULEA VIFARANGA WA UMRI KUTOKA SIKU 1 HADI WIKI YA 4 KWA NJIA YA KISASA;
Mahitaji;
1. Nyumba na vifaa
2. Chakula
3. Tiba ya magonjwa
MAANDALIZI YA NYUMBA/BANDA LA KULELEA WIKI MOJA KABLA YA KULETWA VIFARANGA;
1. Nyumba ya kulelea vifaranga ni lazima ifanyiwe usafi wiki moja kabla ya kuingiza vifaranga.
2. Baada
ya kupigwa deki au kufagiliwa itawekwa dawa ya kunyunyiza na bomba
[sprayer] sakafuni ukutani na upande wa ndani wa paa la nyumba. Dawa hii
itasaidia kuua utitiri, chawa, viroboto na vimelea vya magonjwa
mbalimbali. Dawa itatumika kadri ya maelezo ya watengenezaji.
3. Baada ya kuwekwa dawa liache banda likauke kwa wiki moja kabla ya kuingiza vifaranga.
1. KUTENGENEZA KIFAA CHA KULELEA VIFARANGA (BROODER AND HOOVER;
Hiki ni kifaa maalumu cha kulelea vifaranga wasiotunzwa na mama yao.
Vifaa vya kutengenezea kifaa cha kulelea vifaranga
o Ceiling board na au maboksi magumu
o Wavu /kizuizi cha joto kali
o Chanzo cha joto [jiko la mkaana mkaa, balbu –infra-red bulb]
o Takataka za mbao /mabaki ya mpunga
o Magazeti, / boksi laini
o Mfuniko [hoover].
Kuatamia vifaranga ni mchakato wa kuwapa vifaranga
joto bila kutegemea mama ( joto la balbu au la mkaa) mara baada ya
kutotolewa na mashine hadi pale watakapootesha manyoya au watakopoweza
kukabiliana na mabadiliko ya ujoto /mazingira .
Mahitaji ya msingi ya kuatamia vifaranga kwa kutumia bruda:
Weka joto la kutosha ili kuwafanya vifaranga wakae starehe (bila usumbufu) wakati wa mchana usiku.
Epuka mabadiliko ya kushtukiza ndani ya banda katika kipindi cha wiki mbili za mwanzo baada ya vifaranga kutotolewa.
MASAA MACHACHE KABLA YA KUINGIZA VIFARANGA;
o Jaza maji safi kwenye vyombo ili yapate joto kabla ya vifaranga havijaiingia
o Jaza chakula kwenye vyombo na kudondosha kingine juu ya magazeti
o Tayari yenye mchanganyiko wa sukari na dawa zinazopendekezwa na watalaam.
o Hakikisha chumba kina joto la kadri la nyuzi joto 32.5◦c-35◦c.
MAMBO YA KUFANYA WAKATI VIFARANGA VINAFIKA:
1. Pata idadi yao na kurekodi.
2. Shika mmoja mmoja na kutumbukiza mdomo wake kwenye maji yaliyowekwa dawa na sukari na chick formula.
3. Baada ya hapo chunguza tabia ya vifaranga
ili kuona kama joto lilopo ni sahihi au kuna baridi kali au joto kali .
tabia ya vifaranga :
joto likizidi vifaranga wataachama mdomo , kuhema, na
kutandaza mabawa. Vilevile hula chakula kidogo na hawachangamki na hukaa
mbali na chanzo cha joto(moto)-kigae. Joto likipungua vifaranga
hujikusanya pamoja ubavuni mwa kinga ya joto(moto). Hivyo inampasa
mhudumiaji kuhakikisha anarekebisha joto katika chanzo kulingana na hali
inayojitokeza.
Mambo ya kuzingatia katika kulea vifaranga:
ANGALIA JEDWALI HILI HAPA CHINI.
Umri wa vifaranga [umri katika wiki]
|
Joto linalofaa
|
0-1
|
32.2-35°C(90-95°F)
|
1-2
|
29.4-32.2°C(85-90°F)
|
2-4
|
26.7-29.4°C(84.3-85°F)
|
Chakula: Hakikisha vifaranga wanapewa chakula sahihi na kiasi kile kinachopendekezwa kwa umri na uzito hai husika
Mfano.Wape
chick marsh vifaranga wa siku moja hadi wanapofikia umri wa mwezi mmoja
baada ya hapo watapewa chakula kinachoitwa grower’s marsh/finisher’s
marsh. Usikae zaidi ya masaa mawili (2) kabla ya kuwapa kingine.
usafi:
1.1 Vyombo vya chakula na maji
1.2 Chakula: Hakikisha
chakula safi na maji safi vinapatikana wakati wote. Madini , vitamini
na viuatilifu vinawekwa kadri inavyoshauriwa na waganaga wa mifugo.
1.3 Fanya usafi wa kutosha na kuweka dawa kabla ya kuhamishia kuku bandani
1.4 Mazingira
ya ndani na nje ya banda ni lazima yawe safi na makavu daima kwani
uchafu na unyevunyevu ni chanzo cha vijdudu vya magonjwa kama vile
minyoo na kuhara damu.
Epuka usumbufu (stress) mahali wanapoishi vifaranga ,Mfano:
a) Epuka Kuondoa mfuniko (hoover) wa brooder kila mara.
b) Kubamiza milango kwa nguvu
c) Kuruhusu wageni na kuingia kwenye banda bila mpangilio.
d) Kukaa muda mrefu bila kuwapa chakula
e) Kuwepo kwa joto jingi katika chanzo.
f) Utaratibu usiwe wa kubadilika badilika mara kwa mara mfano chakula na maji.
g) Chunguza
vifaranga kabla ya kwenda kulala na baada ya kuamka . utaratibu
uinaokubalika ni kukesha kwa zamu ili vifaranga wakalaliana na hivyo
kusababisha vifo vyo. Kazi ya kulea vifaranga ni ya kujitolea sana hasa
katika wiki tano za mwanzo.
1.5 mabanda yawe safi na makavu wakati wote ili kuzuia mazalia na chanzo cha maambukizi kutokana na unyevunyevu.
1.5.Mwanga na mzunguko wa hewa wa kutosha:
Kuna Vianzo viwili vya mwanga navyo ni
1. Taa ya kandili/kerosene lamp
2. Taa inayotumia nguvu za umeme- balbu kama vile infrared bulbs.
Mwanga na mzunguko wa hewa ndani ya bruda ni muhimu kwani huvutia na kuvishawishi vifaranga kuanza kula .
Weka madirisha makubwa yenye kuingiza hewa safi na
kutoa ile chafu. Banda lisilo na hewa ya kutosha huchochea kuenea kwa
magonjwa ya mfumo wa hewa. Andaa nafasi ya kutosha ili kuepuka vifaranga au kuku kurundikana.
v Chakula bora na cha kutosha:
a) Wape vifaranga chakula cha kutosha , kizuri na chenye viini lishe vyote .
b) Wape
chakula vifaranfga kwa vipindi vilivyopangwa badala ya kuwapa
mfululizo ili wapate muda wa kutumia chakula walichokula vizuri mwilini.
c) Hakikisha vyombo vya chakula havikai bila chakula
4. Madawa:
Dawa inatakiwa kuwekwa ndani ya chakula na maji ili kuzuia ugonjwa wa kuharisha damu (coccidiosis)
Dawa ya kideri ni vizuri ikatolewa wakati vifaranga wamefika na au siku chache baada ya kuingizwa kwenye brooder.
Vitamin huandaliwa wakati mwingine pamoja na madawa kama antibiotics ili zichanganywe kwenye chakula chao.
Zingatia ratiba ya chanjo inayopendekezwa na wataalamu.
Kuku wapewe dawa ya kuzuia maumivu ya usumbufu kwa siku 2-5.
v Vifaa ndani ya banda la vifaranga:
Vyombo vya chakula:
vyombo vya chakula vitawekwa sehemu ifaaayo na inayofikika na
vifaranga. Hakikisha vifaa havichafuliwi na mavi ya vifaranga au
takataka zilizomo ndani ya banda. Hakikisha unaongeza vyombo vya chakula
na maji kadri vifaranga wanavyozidi kukua na kuongezeka uzito .
Vyombo vya maji :
– ili kazi ya usafi iwe rahisi umbile na ukubwa wa vyombo vya maji viwe
nusu mduara mfano wa muanzi uliopasuliwa katikati. muanzi huu huwekwa
katikati ya vijiti viwili vitakavyoushikilia. Vijiti hivi viwekwe
kattika namna ambayo ni rahishi kuvirekebisha. Vilevile kifaa hiki cha
maji kinaweza kuwekwa kizibo ambacho kitalegezwa au kuondolewa wakati wa
kusafisha. Inashauriwa kuwa vifaa vya kunyweshea viwe na ujazo wa lita
tano. Vilevile vifaa hivi viwe vya plastiki ili kuepuka kuotesha kutu.
Ndoana: hizi ni fimbo za miti au waya ambazo hutmika wakati wa kukamatia kuku kwa ajili ya tiba au kuwauza.
Toroli au mikokoteni :
ikiwa banda limejengwa vizuri , toroli linaweza kusiadia kupunguza
idadi ya masaa yatakayotumika wakati wa kulisha au kuweka maji.
Kuchagua Kundi la vifaranga wenye afya njema:
Chagua vifaranga wenye afya njema ambayo hutambuliwa kwa kuwa na manyoya makavu, macho maangavu na walio wachangamfu.
Chunguza vifaranga wenye kinyeo kilichochafuka na
wazubavu na kisha uwatibu. Vifaranga dhaifu ,wenye vilema na wagonjwa
wagonjwa waondolewe katika kundi la kuku (culling).
Vifaranga wa mayai wahamishiwe kwenye banda la kukulia
wakiwa na umri wa wiki 6-8 ambako watakaa hadi wiki ya 16-18 kabla ya
kuhamishiwa banda la kutagia.
v Mabadiliko ya hali ya hewa:
Wakati wa majira ya joto kuku hupunguza kula , hivyo wakati huu inashauriwa kumwaga maji juu ya paa la banda ili kupunguza joto
.................................................................................................................................................................
.................................................................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment