Fahamu namna ya kutengeneza vyakula vya ng’ombe wa maziwa na ulishaji wake
Baadhi ya vyakula huwa na kiasi kikubwa cha madini kuliko vingine huku lita 10 za maziwa zikiwa na gramu zipatazo 100 za madini.
Iwapo ng’ombe atashindwa kupata kiasi cha gramu 100 za madini kutoka katika chakula alicholishwa kwa siku, atalazimika kutumia madini ya ziada maziwa.
Baadhi ya wafugaji hulisha mifugo yao mchanganyiko wa madini ulioko katika hali ya unga pamoja na chumvi na wanyama huruhusiwa kujipatia mchanganyiko huo kwa kadri wanavyotaka na siyo kawaida kwa mnyama kutumia madini mengi zaidi kuliko mwili wake unavyohitaji.
Ng’ombe wa maziwa anahitajika kulishwa aina ya vyakula vinavyoweza kuupatia mwili wake viinilishe vinavyohitajika kwa ajili ya
- ukuaji,
- nguvu,
- uzazi,
- pamoja na hifadhi ya viinilishe kama
- mafuta,
- protini,
- madini na majimaji.
Kwanini ni muhimu ng’ombe kupata viinilishe?
Ng’ombe huhitaji viinilishe kwa ajili ya kutosheleza mambo yafuatayo;
• Kuufanya mwili udumu katika hali yake ya kawaida, na kuweza kumudu mambo kadhaa muhimu kufanyika kwa ajili ya kudumisha uhai wake ambayo ni pamoja na mapigo ya moyo, kupumua, kutunza joto la mwili, uyeyushaji wa chakula, utoaji wa uchafu mwilini, mzunguko wa damu mwilini. Ili mnyama aweze kuendelea kuishi ni sharti mambo hayo yote yafanyike mwilini mwake hata kama atakuwa amepumzika.
• Kukua, kujengeka kwa mifupa, nyama, mafuta na vitu vingine muhimu mwilini mwake.
• Viinilishe pia huwezesha utengenezaji wa maziwa kwa ng’ombe anayekamuliwa.
• Pia, husaidia katika ukuaji wa ndama tumboni na kuzaa salama kwa ng’ombe mwenye mimba.
1. Dairy meal
Dairy meal ni chakula maalumu cha kusindika cha ng’ombe wa maziwa ambayo hutengenezwa kutokana na mchanganyiko wa vyakula vinavyoweza kuwekwa katika makundi makuu matatu ambayo ni;
• Vyakula vyenye uwezo mkubwa wa kutia mwili nguvu na joto kama vile pumba za nafaka aina ya mahindi, ngano, na mpunga (asilimia 60% hadi 70%).
• Vyakula vyenye uwezo wa kujenga mwili kama vile mashudu ya mbegu za mimea inayotoa mafuta kama vile pamba, alizeti, ufuta, maharagwe (asilimia 25% hadi 35%.
• Vyakula vyenye mchanganyiko wa madini pamoja na chumvi (asilimia 4% hadi 5%).
Mchanganyiko wa molasi na urea ni chakula kizuri cha wanyama wanaocheua na hulishwa kama nyongeza ya malisho na vyakula vinavyompatia mnyama nguvu, protini pamoja na madini.
Nitrojeni kutokana na urea iliyopo kwenye mchanganyiko huu ni muhimu sana kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya mwili ikiwa ni pamoja na kuujenga mwili na kutengeneza maziwa kwa wanyama wanaonyonyesha. Kwa kawaida mwili hupata nitrojeni kwa kuyeyushwa vyakula vya protini vilivyoliwa na mnyama.
Aidha, vipo baadhi ya vyakula vya ziada ambavyo ingawa havina protini bado vina uwezo wa kuupatia mwili wa mnyama naitrojeni na mojawapo ya vyakula hivyo ni mchanganyiko wa molasi na urea.
Wanyama wanaocheua wanaweza kujipatia nitrojeni kutoka kwenye mchanganyiko wa molasi na urea kwa kutumia vijidudu vilivyomo kwenye matumbo yao.
Namna ya kulisha changanyiko wa molasi na urea
Kuwapa wanyama jiwe maalumula kulamba lililotengenezwa kwa kutumia urea na molasi.
Kuchanganya molasi na urea kwenye malisho makavu kwa kunyunyizia na kuchanganya kwa makini ili iweze kushikana vyema na malisho hayo.
Athari zinazoweza kutokea kwa kuchanganya molasi, urea na maji
• Urea iliyopo kwenye mchanganyiko hupungua kwa sababu kiasi fulani cha naitrojeni hupotea hewani. Urea inapochanganywa na maji, kiasi cha hewa ya amonia hujitengeneza na kwa kiasili kimojawapo cha hewa hiyo ya amonia ni naitrojeni na hewa hii hupotea hewani mara inapojitengeneza na hivyo kuchangia kupotea kwa naitrojeni ambayo ilitakiwa kuingia mwilini mwa mnyama.
• Mara nyingi wanyama hunywa maji mengi kwa mkupuo mmoja huku mchanganyiko wa molasi na urea ukitakiwa uingie mwilini mwa mnyama taratibu. Hii husaidia kutoa nafasi kwa ini la mnyama kuondoa masalia yasiyotakiwa kwenye damu baada ya naitrojeni kutolewa kutoka kwenye urea.
Ini lisipofanya kazi ya kuondoa masalia haya kila mara yanapojijenga au yanapokuwa mengi kuliko uwezo wa ini kuweza kuyaondoa, basi mwili wa mnyama unaweza kuathirika na hata kifo kutokea.
Kutokana na ukweli kuwa kwa kawaida kasi ya mnyama kula malisho makavu ni mdogo, basi kasi ndogo ya ulaji wa malisho makavu yaliyotiwa mchanganyiko wa molasi na urea huenda sambamba na utoaji wa masalia ya urea kwenye damu na kumsaidia mnyama kutodhurika anapolishwa malisho makavu yenye mchanganyiko huu.
Aidha katika unywaji wa maji, kasi ya mnyama kunywa maji ni kubwa mno hasa ukilinganisha na kasi ya utoaji wa masalia ya urea kwenye damu, hivyo ni dhahiri kuwa masalia ya urea ambayo hutumiwa na mnyama huyo kwenye maji huweza kubaki kwenye damu kwa muda yakisubiri kuondolewa na hivyo kusababisha madhara au kifo kwa mnyama.
• Vipimo maalumu vya kulisha vinapendekezwa kufuatana na aina ya mnyama, umri wake na uzoefu wa kutumia mchanganyiko huu. Iwapo mchanganyiko huu utawekwa kwenye maji, ni vigumu kutambua kila mnyama ametumia kiasi gani hasa pale chombo kimoja kinapotumika kuwanywesha maji wanyama zaidi ya mmoja.
Namna ya kuepuka athari hizi
• Kwa wanyama wanaokula haraka, ni vyema kutokuchanganya mchanganyiko huu na vyakula vya kusindika kama vile dairy meal, mashudu ya mbegu mbalimbali za mafuta na pumba za nafaka aina nyingi, kwani wanyama hupenda kuvila kwa haraka na vinapoongezewa mchanganyiko huu huwa vitamu zaidi na kasi ya ulaji huongezeka pia.
• Hakikisha wanyama wanaolishwa mchanganyiko huu ni wale tu wanaocheua ambao tangu waachishwe maziwa ni miezi miwili imepita au tayari ni wakubwa.
3. Jiwe la kulamba lenye mchanganyiko wa molasi, urea na madini
Ni rahisi sana kutengeneza jiwe la kulamba lenye mchanganyiko wa molasi, urea na madini, ambalo husaidia wanyama kuongezea miili yao nguvu na viinilishe muhimu ambazo huweza kuwa pungufu katika kipindi fulani cha mwaka ambazo ni protini na madini.
Ingawa ng’ombe mkubwa anatakiwa amalize ½ kilo ya jiwe la aina hii kwa siku, mara nyingi inakuwa vigumu kulimaliza hivyo ni muhimu kuzingatia njia nzuri ya kutengeneza jiwe litakalomsaidia mnyama kupendelea kulilamba mara kwa mara na hivyo kulitumia kwa kiasi kikubwa.
Ni vyema kutumia pumba iliyosagwa kikamilifu na kuwa laini kiasi cha kutosha ili mnyama anapolamba jiwe hili asibakiwe na chengachenga mdomoni. Jiwe hili pia hutakiwa kuwa gumu ili wakati mnyama anapolamba kusiwepo na kiasi chochote kitakachopotea.
Ni muhimu pia kutumia kiasi halisi cha bentonite na urea kilichopendekezwa kwani urea ikizidi inaweza kuleta madhara au kifo kwa mnyama na bentonite ikizidi pia inafanya jiwe kuwa gumu mno na hivyo kumfanya mnyama ashindwe kutumia kama inavyotakiwa.
Namna ya kulitengeneza jiwe
Kabla ya kuanza kutengeneza jiwe, ni muhimu ukaandaa vifaa na malighafi zote zinazohitajika yakiwa katika uwiano sahihi.
Malighafi
Molasi kilogramu 35, urea kilogramu 15, madini/bone meal kilogramu 2, chumvi kilogramu 5, bentonite kilogramu 13 na ngano/mchele uliosagwa kilogramu 30. Maji pia yatatumika
ikiwa mchanganyiko utakuwa mgumu (kwa kila kilogramu 1 hadi 3 weka asilimia 1 hadi 3).
Vifaa
Chombo cha kuchanganyia kama sufuria, mwiko wa kukorogea au mti mgumu, fremu au vibao ulivyovitengeneza
kulingana na maumbo unayoyataka.
Hatua
• Weka kiasi cha molasi ulichopima katika chombo ulichoandaa kwa aji ya kutengenezea jiwe.
• Ongeza urea na kisha changanya kwa kukoroga hadi ichanganyike vizuri.
• Weka madini, fuatisha chumvi na bentonite kisha endelea kuchanganya kikamilifu.
• Baada ya kuchanganya, ongeza mchele au ngano na kisha endelea kukoroga hadi vichanganyike vizuri.
• Mimina mchanganyiko kwenye fremu za mbao ulizoziaandaa kufuatana na umbo la jiwe unalolitaka.
• Baada ya kumimina mchanganyiko kwenye fremu, acha kwa muda wa siku 2 au 3 ili ukauke vizuri kabla ya kuanza kulitumia.
Kumbuka: Kilo 100 za mchanganyiko huu zinaweza kutengeneza mawe 30, kila moja likiwa na uzito wa kilo 3.3 na ukubwa wa sentimita 10 X 20 x 6 (yaani upana wa sentimita 10, urefu wa sentimita 20 na kimo cha sentimita 6).
4. Madini na chumvi
Kutegemeana na ukubwa wa mnyama na aina ya chakula kinacholishwa kwa siku, mnyama anaweza kuhitaji kiasi cha gramu 10 hadi 50 za madini kwa siku ili kutosheleza mahitaji yake ya mwili.
Baadhi ya vyakula huwa na kiasi kikubwa cha madini kuliko vingine huku lita 10 za maziwa zikiwa na gramu zipatazo 100 za madini.
Iwapo ng’ombe atashindwa kupata kiasi cha gramu 100 za madini kutoka katika chakula alicholishwa kwa siku, atalazimika kutumia madini ya ziada kutoka mwilini mwake ili kutengeneza maziwa.
Baadhi ya wafugaji hulisha mifugo yao mchanganyiko wa madini ulioko katika hali ya unga pamoja na chumvi na wanyama huruhusiwa kujipatia mchanganyiko huo kwa kadri wanavyotaka na siyo kawaida kwa mnyama kutumia madini mengi zaidi kuliko mwili wake unavyohitaji.
Namna ya kutengeneza mchanganyiko wa madini
Ikiwa unaweza kupata chumvi ya kawaida, madini yaliyoko katika hali ya unga kama vile chokaa, basi unaweza kujitengenezea mwenyewe mchanganyiko wa madini kwa ajili ya mifugo.
Mchanganyiko huo wa madini utakuwa na gharama nafuu zaidi na utaweza kulisha kati ya gramu 20 hadi 100 kwa siku kwa ng’ombe wa umri wowote.
Pili, kama huwezi kupata mchanganyiko huo, basi unaweza ukatafuta fosifeti na kuichanganya na mifupa iliyosagwa vizuri pamoja na chumvi (ikiwezekana upate chumvi yenye iodine).
Tatu, ikiwa njia zote mbili hapo juu utazishindwa basi unaweza kuchanganya chumvi na mifupa iliyosagwa pekee na kulisha ng’ombe kila siku.
................................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment