script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X





CHAKUA CHA AZOLLA

Azolla ni nini?
Azolla ni mimea inayoelea ktk maji water ferns.
Mimea hii iko mfano wa magugu maji lakini yenyewe ni midogo midogo yenye mizizi inayoelea majini.
Kwanini Azolla ni maarufu?
Azolla imejipatia umaarufu kwasababu inapunguza gharama za ulishaji mifugo kwa wastani wa 80-100%.
Pia Azolla ina virutubisho vingi mifugo inahitaji kwa makuzi yao na uzalishaji bora ukilinganisha na vyakula tunavyotengeneza majumbani au mashineni.
Pia Azolla ina manufaa makubwa ktk kilimo katika kufanya  Nitrogen Fixation  katika mashamba ya mpunga na hapa ndipo Azolla hutumika kama  bio-fertilizer  na  green manure  ktk mashamba ya mpunga.
Azolla inazalishwa wapi?
Azolla huzalishwa ktk mabwawa, vyombo mbalimbali mfano mabeseni na ktk mashamba ya mpunga.
Aina za Azolla
Hizi ni aina za azolla:
1. Azolla Pinnata
2. Azolla Caroliniana
3. Azolla Mexicana
4. Azolla Rubra
5. Azolla Microphylla
Na nyingine nyingi.
Virutubisho katika Azolla
Azolla ina wingi wa protini, amino acids, vitamins, dry matter, lipids, minerals (kama magnesium, calcium, phosphorous na pattasium). Pia azolla huzalisha wanga (carbohydrates)
Utengenezaji wa Bwawa la Azolla
#Bwawa la Azolla lichimbwe katika urefu na upana  kulingana na kiasi gani mfugaji anataka kuzalisha kwa siku na pia eneo lake.
# Kina cha bwawa kiwe 30cm
# Bwawa lijengwe kwa cement, turubai au nailoni ili kuzuia upotevu wa maji
# Bwawa liwekewe kivuli kwa juu  (partial shades)  au lichimbwe chini ya miti au sehemu yenye kivuli. Azolla inahitaji  jua  kwa wastani wa 50%.
# Bwawa liwekewe fensi kuzuia mifugo na watu wasiohusika kuingia
Uzalishaji bora wa Azolla
Baada ya maandalizi bora ya bwawa la Azolla kukamilika, upandaji uzingatie yafuatayo:
# Udongo wenye rutuba na mbolea mbichi ya samadi katika uwiano sawa (Ratio ya 1:1) uchanganywe pamoja na kusambazwa ndani ya bwawa. Pia ni vizuri ukiweka na mbolea za viwandani mfano TSP au YaraMila Unik 17.
#Kisha maji yafunguliwe kujaza bwawa, maji yawe katika kina cha 5-10cm kutoka usawa wa udongo na mbolea
# Kisha maji yaachwe yatulie kwa masaa 1-2. Baadaye povu lote linaloelea litolewe
# Kisha mbegu ya Azolla ioandwe kwa kurushia na kusambaza pande zote za bwawa. Kilo za mbegu ya Azolla hutegemea ukubwa wa bwawa. Ipandwe katika uwiano wa 1:2 (Ratio ni 1:2)
# Baada ya kupanda bwawa enye Azolla liachwe kwa muda wa siku 14, hapo litakuwa limejaa. Na hapo ndipo mfugaji ataruhusiwa kuanza kuvuna Azolla kwa ajili ya mifugo yake. Wastani wa 1kg ya azolla itavunwa ktk kila 2m ya bwawa kwa siku.
# Baada ya kuanza kuvuna ndipo uboreshaji wa bwawa unaanza. Kila baada ya wiki 2 mbolea ya samadi mbichi iliyochanganywa na TSP au YaraMila Unik 17 itawekwa ktk bwawa kulingana na vipimo vya ukubwa wa bwawa ili kuliboresha bwawa
#Azolla inakuwa na kujizalisha kwa haraka sana katika maji yenye PH 4.5-7 na joto 20-35°C. Joto zaidi ya 36°C linaathiri sana uzalishaji wa Azolla.
#Bwawa la Azolla linatakiwa kubadilishwa maji mara 1 kila baada ya miezi 6-8 na uzalishaji kuanza upya
Baada ya Azolla kuvunwa na kabla ya kupewa mifugo ni lazima ioshwe kwa maji safi na salama, na kisha ndio mifugo ipewe.
Azolla inalishwa kwa Poultry na Livestock
Vitu vinavyoathiri uzalishaji wa Azolla
1. Joto kali (High Summer Temperature)
2. Joto dogo zaidi ( Extreme Low Temperature)
3. Ukosefu wa maji (Water Scarcity)
4. Unyevu mdogo ( Low Humidity)
5. Maji yasiyo na ubora ( Poor Quality of Water)

NOTE
Haya yote kuhusu Ufugaji pia unaweza kuyapata kupitia Website yetu ya www.mshindoveterinarycentre.com
...................................................................................................................

0 comments:

 
Top