SAMAKI HUKUA HARAKA WAKIPATIWA CHAKULA KILICHO BORA
SAMAKI HUKUA HARAKA WAKIPATIWA CHAKULA KILICHO BORA : Si jambo rahisi kupata Vyakula vya samaki vinavyozalishwa viwandani katika ukanda huu wa Afrika mashariki kwa vile sekta hii ndiyo inaanza kukua. Na hata mahali ambapo makampuni yanajihusisha na biashara ya samaki basi huzalisha chakula kwa ajili ya matumizi yake na ziada huweza kuuzwa kwa wafugaji wengine. Na mara nyingi
vyakula hupatikana kikiwa cha aina mbalimbali mathalani chembechembe (pellets) vikavu, vya chakula vya chembechembe zinavyoelea majini (Floating feeds pellets) au chembechembe za chakula vinavyozamishwa majini.
UTAYARISHAJI WA CHAKULA:
TENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI MWENYEWE
Mfugaji anaweza kupunguza gaharama za kununua chakula kwa ajili ya samaki, kwa kutengeneza chakula mwenyewe kwa kutumia malighafi alizo nazo katika eneo lake. Tumia resheni rahisi ambayo itakupatia chakula cha kutosha na kwa gharama nafuu.
MAHITAJI
• Pumba ya mahindi sadolini 1.
• Pumba ya ngano au mpunga sadolini 1.
• Dagaa sadolini 1.
• Kilo moja ya soya.
• Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti.
NAMNA YA KUANDAA
• Changanya malighafi hizo kwa pamoja.
• Saga hadi zilainike.
• Kanda kama vile unga wa kutengenezea chapati.
• Weka kwenye mashine ya kusaga nyama au kutengenezea tambi.
• Anika kwenye jua la wastani.
• Baada ya kukauka, vunja vunja kwenye vipande vidogo vidogo kama inavyoonekana pichani hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia kuwalisha.
• Tumia lishe hiyo kwa samaki mara tatu kwa siku.
Baadhi ya wafugaji wameweza kutumia chakula walichotayarisha wenyewe na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Mfano wa michanganyiko ya vyakula ambavyo vimekuwa rahisi kutumia na kuwapatia tija wafugaji hujumuisha:
• Mchanganyiko wa asilimia 76 pumba za mpunga na asilimia 24 dagaa
• Mchanganyiko wa samaki aina ya uduvi wanaopatikana kutoka maji matamu (Caradina spp) na pumba za mahindi.
Uchakataji wa vyakula hivi hupitia hatua mbalimbali kama vile usagaji, uchanganyaji, ugandishwaji pamoja, uongezwaji kidogo wa mafuta, kupoozwa na kukatwakatwa vipande vidogovidogo. Katika ukanda wa Afrika Mashariki vyakula vingi vinavyotayarishwa mashambani hufanywa kwa zana duni ambazo hutumia nguvu za binadamu au kuendesha kwa mashine na huzalisha chini ya magunia 5 ya kilo 90 kila moja kwa siku.
Virutubisho vya chakula husagwa kwa mikono na baadaye huchanganywa kwa kutumia mashine ya mkono ya kuchanganyia kasha baada ya hapo hutengenezwa kuwa vipandepande (pellets) na mashine maalum kwa kazi hiyo,
• Kwa kuanzia tupia kwenye bwawa lako kiasi kidogo cha chakula wakati fulani wa siku na chunguza kuona kama samaki wako watakifuata
chakula.
chakula.
• Baada ya samaki kukikubali chakula kilichotayarisha na kufahamu watakuwa wakikipokea toka upande upi wa bwawa, basi watazidisha hamu ya kukila na kwa kawaida samaki hutumia dakika 15 kula na kukishiba chakula.
Inapasa uwe umejiandaa kpunguza kiasi cha chakula unachowapatia samaki wako kwa siku pale moja kati yafutayo yakitokea:
• Inapodhihirika samaki wanashindwa kukila chakula kwa kiasi ambacho wamekizoea kukila
• Joto la maji linapokuwa limepanda kuliko kawaida kwa kipindi chote cha mwaka.
• Kiwango cha hewa safi (oxygen) ndani ya maji ni kidogo.
Hapa itabidi ielewekwe kwamba haya yote matatu yanaweza kutokea kwa wakati mmoja wakati unakaribia mwisho wa mzunguko wa uzalishaji na hasa unapopanga kipindi chako cha uvunaji kuwa msimu wa joto kali.
Zingatia dondoo zifuatazo unapowalisha samaki wako kila siku:
• Samaki aina ya perege huwa na matumbo madogo na huchunga kutwa nzima kutafuta chakula
• Muda muafaka wa kuwapatia chakula cha ziada ni kati ya saa 4 asubuhi na saa 10 jioni wakati ambao kiasi cha hewa safi kilichopo majini na joto vinapokuwa katika kiwango cha juu kidogo.
• Inashauriwa kuwalisha samaki wako kwa kutumia sehemu na wakati moja kwa kila bwawa. Hii itawafanywa wajenge mazoea ya haraka kujua muda ambao watatarajia kupata chakula kizuri.
• Mlishaji samaki anapasa kuwa mtu anayepatikana kwa uhakika na anayejituma.
ULISHAJI KWA KUTUMIA MIKONO UNA FAIDA:
Baadhi ya njia ambazo hutumika kuwapatia chakula samaki hujumuisha zifuatazo:
• Kukirusha chakula kwenye maji bwawani wakati akitembea pembezoni mwa bwawa.
• Weka chakula kwenye jukwaa la kulishia au meza ambazo huwa hujengwa ndani ya maji
• Tumia malishio maalum (demand feeder) ambalo huruhusu chakula kutoka wakati samaki analipogonga (lever).
• Tumia malishio yanayojiendesha yenyewe (automatic) ambayo huweza kusambaza au kukiruhusu chakula kutoka kwa muda maalum
uliopangwa.
uliopangwa.
• Itapaswa ielewekwe kwamba aidha mfugaji anatumia demand au automatic feeder inapasa mhudumiaji awepo wakati wa samaki kula na
malishio haya yanahitaji kujazwa chakula mara kwa mara na kipindi fulani cha siku. Na ni vema kuwa yanachunguzwa mara kwa mara ili kuhakikisha yanafanya kazi vizuri.
malishio haya yanahitaji kujazwa chakula mara kwa mara na kipindi fulani cha siku. Na ni vema kuwa yanachunguzwa mara kwa mara ili kuhakikisha yanafanya kazi vizuri.
• Faida kubwa ya kulisha samaki kwa kutumia mikono humsaidia mfugaji kutambua kwa kiasi gani samaki wake wanakula vyema chakula
na kwa kasi gani wanakuwa na dalili zozote za samaki kutokula chakula kwa hamu ni ishara ya kuwa pengine kuna tatizo limetokea
na kwa kasi gani wanakuwa na dalili zozote za samaki kutokula chakula kwa hamu ni ishara ya kuwa pengine kuna tatizo limetokea
ZIFUTAZO NI SABABU ZINAZOSABABISHA SAMAKI WAKO WA AINA YA PEREGE WASILE CHAKULA SAWASAWA:
• Maji ni ya baridi mno
• Inawezekana kuna baadhi ya samaki wamekufa
• Chakula ni kizito kiasi cha kuzama haraka kwenye maji na hivyo siyo rahisi kutambua kama samaki wamekila.
• Mgao wa chakula ulioonyeshwa kwenye jedwali hapo chini unaweza kutumiwa kwa bwawa linalofugwa samaki wa aina ya perege au
kwenye bwawa linalofugwa perege na kambale (Polyculture).
kwenye bwawa linalofugwa perege na kambale (Polyculture).
• Mgao huu unaweza kulishwa samaki mara moja kwa siku au unaweza ukagawanywa mara mbili na kulishwa asubuhi na sehemu iliyobaki jioni.
• Kwa kuweza kupata ubora wa chakula unachiwalisha samaki wako ni vema ukapima uzito wa sampuli inayowakilisha samaki wote bwawani kila baada ya wiki mbili kuweza kujua uzito wao halisi ambao utakusaidia kupanga kiasi cha chakulakuwalisha kuliko kutumia uzito wa makadirio
............................................................................................................................DOWNLOAD APP ZETU HAPA TOKA MSHINDO MEDIA
0 comments:
Post a Comment