script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X







1. SIFA ZA NG’OMBE WA MAZIWA


x Umbo lililopanuka kwa nyuma na kupungua kuelekea kichwani
x Mgongo ulionyooka kuanzia mabegani kuelekea mkiani
x Miguu mirefu iliyonyooka, minene yenye kuacha nafasi kwa ajili ya kiwele na kwato imara
x Kiwele kiwe kikubwa chenye chuchu nne, ndefu, na unene wa wastani
x Nafasi kati ya chuchu na chuchu iwe ya kutosha
x Endapo ng’ombe anakamuliwa awe na kiwele kikubwa kilichoshikamana vizuri mwilini, na mishipa mikubwa kwenye kiwele iliyosambaa
x Aina ya ng’ombe wa maziwa wanaofugwa kwa wingi nchini ni pamoja na Friesian, Ayrshire, Jersey, Mpwapwa, Simmental na chotara watokanao na mchanganyiko wa aina hizo na Zebu.

Ng’ombe anayekamuliwa anahitaji kupata chakula kwa ajili ya kujikimu na cha ziada kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa. Ili kukidhi mahitaji ya uzalishaji wa maziwa ng’ombe:
x Apewe chakula cha ziada kwa kiwango cha kilo 1 kwa kila lita 2-3 za maziwa anayotoa,
x Apewe madini na virutubisho vingine kulingana na mahitaji,
x Apewe maji mengi kwa vile ni ya muhimu katika kutengeneza maziwa,
x Aachwe kukamuliwa siku 60 kabla ya kuzaa. Uachishwaji huu ufanywe taratibu ili ifikapo siku ya 60 kabla ya kuzaa ukamuaji usitishwe,
x Baada ya kusitisha kukamuliwa, apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku hadi atakapozaa; na
x Apatiwe kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.

3. UZALISHAJI WA MAZIWA
Lengo la ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ni kupata maziwa mengi, safi na salama pamoja  na mazao yatokanayo na maziwa.
Mambo muhimu ya kuzingatia ni:-
x Sehemu ya kukamulia iwe safi na yenye utulivu,
x Ng’ombe awe na afya nzuri, msafi na kiwele kioshwe kwa maji safi ya uvuguvugu
x Mkamuaji awe msafi, kucha fupi na asiwe na magonjwa ya kuambukiza,
x Inashauriwa mkamuaji asibadilishwe badilishwe,
x Vyombo vya kukamulia viwe safi
x Muda wa kukamua usibadilishwe; na
x Maziwa ya mwanzo kutoka kila chuchu yakamuliwe kwenye chombo maalum (strip cup) ili kuchunguza ugonjwa wa kiwele.
Maziwa yahifadhiwe vizuri katika mitungi (milk can), kabla ya kufikishwa sokoni

3. MAMBO YA KUZINGATIA
x Ng’ombe apate mimba akiwa na miezi 15.
x Mtoto wa kwanza akiwa na miezi 24.
x Ndani ya miezi 3 baada ya kuzaa apate mimba nyengine.
x Asilimia 60% ya ng’ombe wote katika shamba lazima wawe na mimba wakati wote.
x Ng’ombe anayekamuliwa akaushwe akiwa na mimba ya miezi 7 na apewe chakula kizuri cha ziada kwa miezi miwili kabla ya kuzaa

MATATIZO
x Upungufu wa madini (lack of minerals), ng’ombe mwenye upungufu wa madini anachelewa au kutoingia kabisa katika joto.
x Pia mimba hazishiki hata akipandishwa.
x Magonjwa sugu, Hakikisha muda wote ng’ombe anakuwa na katika afya nzuri ili kupata mazao bora na ya uhakika.


0 comments:

 
Top