Uhamilishaji (AI) ni njia bora ya kuboresha ng’ombe wako. Chagua mbegu kwaajili ya ng’ombe wako kutokana na utakavyomtumia ndama.
Kama unataka maziwa mengi utahitaji kuzalisha kwaajili ya:
- Kiwele kizuri( imara, mraba na chuchu zenye nafasi vyema)
- Miguu mizuri ( iliyonyooka, mipana na imara)
- Uzalishaji mzuri( huzalisha kiurahisi, kuzaa kirahisi)
Mpigie simu mtaalamu wako wa mifugo mara tu unapoona dalili za ng’ombe kuwa na joto. Ng’ombe wako lazima ahudumiwe masaa 12-18 baada ya kuona uke uliovimba na ute msafi. Unapoona damu, umeshachelewa. Ng’ombe wako alikua kwenye joto siku 3 zilizopita. Itabidi ungoje mpaka siku 18-22 zijazo za joto kabla ya kufanya uhamilishaji.
Angalizo: Kama uchafu ni mweupe, njano au una harufu, mpigie simu mtaalamu wako. Ng’ombe wako anaweza kuwa na maabukizi.
Utunzaji Kumbukumbu
Uwekaji kumbukumbu wa ng’ombe wako unasaidia kufatilia afya na uzalishaji wa ng’ombe wako.
- Utajua wakati atakua na joto. Angoja siku 45 baada ya ng’ombe wako kupata ndama, uwe unaangalia uke uliovimba na uchafu msafi.
- Epuka kurudia uzalishaji kwa kunakili mbegu gani ulitumia kwaajili ya uhamilishaji.
- Kama
unauza ng’ombe wako, mnunuzi ataulizia kuona kumbukumbu zako ....................................................................................... DOWNLOAD APP ZETU HAPA TOKA MSHINDO MEDIA
0 comments:
Post a Comment