script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X





 Mshindo Media
Mshindo Media
Mbwa ni mnyama muhimu sana katika maisha ya binadamu kwani mnyama huyu husaidia katika ulinzi na mapambo katika nyumba, hivyo basi kumtunza mbwa ni jambo la msingi sana ikiwemo udhibiti wa magonjwa na wadudu wasumbufu pamoja na maradhi bora(nyumba/banda), hivyo basi yafahamu magonjwa na wadudu wasumbufu wanaosumbua mbwa kwa sana.


 1. KICHAA CHA MBWA  (RABIES) 
Kichaa cha mbwa ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoambukizwa kutoka kwa wanyama hadi binadamu kupitia kwa mate,kwa kung`atwa na mbwa mwenye maambukizi ya virusi vya kichaa. Ambapo mbwa au mnyama aliye patwa na virusi hivi akimng`ata mtu au mnyama mwingine asiye kuwa na kichaa umuambukiza.
Kichaa hupatwa kwa wanyama walio kundi la mamalia,kwa paka wao wanaukinzani kidogo na ugonjwa huu kulinganisha na mbwa.
Mara baada ya kuumwa waweza usione dalili za ugonjwa huu,kwani uchukua muda, kulingana na sehemu uliyo umwa hadi kufikia katika ubongo.

Dalili za awali za kichaa cha mbwa.
(a) Mbwa kujikuna mara kwa mara.
(b) Mbwa kutokwa na mate mengi mdomoni.
(c) Mnyama kupoteza hofu ya kitu chochote.
(d) Mnyama kung`ata vitu ovyo ovyo.
(e) Mnyama kuzunguka ovyo
(f) Mbwa kutependa mwanga na kukaa gizani.
(g) Mbwa kuogopa maji.
(h) Mbwa kuogopa mwanga.
(i) Mbwa kubadili tabia,mbwa mkali kuwa mpole na mpole kuwa mkali ( mbwa huwa na tabia zisizo za kawaida.)
(j) Mbwa kukojoa mara kwa mara.
(k) Mbwa kutopenda vitu halivyovizoea.
Dalili za baadae za kichaa cha mbwa.
(a) Mnyama kupoteza fahamu.
(b) Mnyama kupooza baadhi ya viungo.

 KUDHIBITI
(a) Mpatie mbwa wako chanjo kila baada ya muda wa mwaka mmoja.
(b) Kwa mbwa waliokwisha pata kichaa cha mbwa hakikisha wanadhibitiwa vya kutosha, kwani mbwa waliopata kichaa huchukua siku tatu hadi kufa.
(c) Dhibiti mbwa wanaozulula mtaani (zuia mbwa wa mtaani.)
(d) Jina la chanjo ni  RABIES .

 2. UGONJWA WA MFUMO WA HEWA. 
Huu ni ugonjwa unao athiri mfumo wa hewa ikiwemo TB,Phnemonia, ni magonjwa yanayo sambaa kutoka mnyama mmoja kwenda mnyama mwingine kwa njia ya hewa.

 Dalili zake,
a) Upumuaji wa shida.
b) Mbwa kushidwa kupumua.
c) Kupumua kwake kunatoa sauti nzito, ule wa kukoroma.
d) Mbwa kukohoa.
e) Mbwa hupumzika mara kwa mara.
f) Mbwa kutoweza kubweka.
g) Kutoka mapovu puani au ute.

Tiba.
h) Mpatie mbwa wako dawa yeyote ya Antibiotics kama; *Otc,Penstrep,Tylosin* .
i) Pamoja na dawa ya vitamini ambayo itamsaidia kurudisha hamu ya kula.

 3. MINYOO (WORMS) 
Minyoo ni wadudu wanaosumbua kwa kiasi kikubwa sana katika mbwa hata kwa wanyama wengine wengi wafugwao kama mbuzi,ng`ombe na kondoo, ambapo huweza sababisha madhara makubwa katika mbwa na kupelekea mbwa kudumaa na hadi kufa.

 Dalili za Minyoo
a) Kuharisha.
b) Mbwa kupoteza hamu ya kula.
c) Manyonya kusambaratika.
d) Uzito kushuka.
e) Mbwa kuwa dhaifu.
f) Mbwa kukohoa

Wafuatao ni aina ya minyoo wanaosumbua sana katika mbwa.
1. Minyoo wa mviringo.
2. Minyoo wa kwenye moyo.
3. Minyoo wa kwenye mapafu.

 Tiba.
Fanya chanjo za minyoo kwa kila baada ya muda wa miezi mitatu, na kwa wale ambapo tayari wamepata ugonjwa wa minyoo wapatiwe dawa ya minyoo ambayo ni IVEMECTIN.

 4. UKURUTU (MANGE) 
Ugonjwa wa  ngozi,na ugonjwa huu uweza kutoka kwa mnyama mmoja kwenda mnyama mwingine,pia hata kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.

 Dalili .
a) Mbwa kujikuna kupita kiasi.
b) Manyoya kunyonyoka.
c) Gamba gumu ujitengeneza juu ya ngozi.
d) Eneo liliathirika huwa na gamba gumu.
e) Mnyama anakuwa anajikuna mara kwa mara.
Udhibiti.
a) Ogesha mbwa wako mara kwa mara angalau mara tatu kwa kila mwezi,hii itasaidia mbwa kutopata ugonjwa wa ukurutu.
b) Tenga mbwa waliopatwa na ukurutu.
c) Kwa mbwa waliopata tayari ukurutu wapatie dawa ya IVEMECTIN dawa hii imeonesha mafanikio makubwa katika kutibu ukurutu na dawa hii uchomwa katikati ya ngozi na nyama.

 5. UGONJWA WA KUTETEMEKA (CANINE DISTEMPER). 
Huu ni ugonjwa unaosambaa kutoka mnyama mmoja kwenda mwingine,na ni ugonjwa unapelekea vifo vya mbwa wengi.Ni ugonjwa wenye chanjo zake.
Ugonjwa huu usababishwa na virusi wanaoitwa Canine Distemper Virus(CDV)

 Dalili za Ugonjwa .
a) Mgonjwa kutetemeka
b) Mbwa kupooza miguu ya nyuma.
c) Anapunguza kula.
d) Macho yanavimba hadi upofu.
e) Ute ute mwingi kutoka kwenye pua.
f) Kuharisha
g) Dalili ya mwisho mbwa kupooza mwili
Udhibiti.
a) Ugonjwa huu hauna tiba bali ni chanjo inayoitwa DHLP.
b) Chanjo hii apewe mbwa akiwa na umri wa wiki 8 hadi wiki 12.

 6.WADUDU WASUMBUFU 
Mbwa akiwa na wadudu hawa hujikuna sana na hujikuna mara kwa mara hasa hasa sehemu za mkia, pia mbwa hukosa raha na muda mwingi hupoteza hadi hamu ya kula kwa usumbufu huu wa wadudu, wadudu hawa sumbufu ni kama viroboto, kupe, chawa na papasi.

 Udhibiti .
- Jinsi ya kudhibiti wadudu hawa ni kuogesha kwa kutumia dawa maalumu Dog shampoo, tik tik na paranex. Kwa dog shampoo imeonyesha kufanya vyema sana kwa kudhibiti na kuua kabisa.
- Usafi wa nyumba wanazo ishi mbwa ni muhimu sana kwa huku ndiko kama usafi usipo zingatiwa wadudu hawa uzaliana kwa wingi sana, safisha kwa maji safi pamoja na kutumia dawa maalumu ili kudhibiti wadudu hawa, hakikisha dawa unachanganya kwa usahihi bila kudhidisha dawa kwani uweza pelekea mbwa  kudhurika.

7. VIRUSI VYA PARVO .
Ugonjwa huu (virusi vya parvo) uwakumba sana watoto wa mbwa wenye umri wa kuanzia wiki 2 hadi wiki 4.Husababishwa na virusi aina ya Canane parvo virus

 Dalili :
a) Kuharisha.
b) Kutapika.
c) Wanakosa hamu ya kula.

 Tiba .
a) DHLP ni chanjo inayotumika kudhibiti ogonjwa huu.
b) Antibiotic kama OTC hutumika kwa kutuliza tu na sio kutibu magonjwa.

0 comments:

 
Top