Mshindo Media |
I. MINYOO YA NG'OMBE.
Ugonjwa wa minyoo husababisha hasara kwa mfugaji wa ng'ombe . Utafiti unaonyesha kuwa ng'ombe wengi wanaathirika na minyoo hiyo hupunguza uzalishaji. Aidha utafiti unaonyesha kuwa tatizo la minyoo kwa ng'ombe limeenea hapa nchini kwetu.
AINA ZA MINYOO.
- Minyoo inayoathiri ng'ombe imegawanyika katika makundi mbalimbali kama ifuatavyo;
- Minyoo inayoishia kwenye maini ya ng'ombe (liverflukes).
- Minyoo inayoishia kwenye mapafu (lungworms).
- Minyoo mikubwa ya mviringo (large roundworms).
- Minyoo midogo ya mviringo (small roundworms).
Dalili za ng'ombe mwenye minyoo.
- - Kupoteza uzito
- - Kukosa hamu ya kula
- - Kuhara
- - Kupungukiwa na damu
- - Kuwa na homa
- - Afya yake kufifia na hatimaye kufa
- - Tumbo kuwa kubwa kupita kiasi (ndama).
Namna ya kudhibiti.
Wanyama wapewe dawa za kutibu minyoo mara kwa mara.
Mfano:
- NILZAN
- NILVERM
- PIPERAZINE
- ANACUR
- THIABENDAZOLE
- YOMESAN
- OXYDOZIDENE
Madhara ya minyoo.
- Husababisha upungufu wa damu.
- Husababisha upungufu wa maziwa.
- Ng'ombe huweza kufa.
Unataka kujua ni magonjwa gani mengi ambayo huathiri ng'ombe kwa kiwango kikubwa? Usikose kusoma hapa tena siku ya kesho.
0 comments:
Post a Comment