NAMNA YA KUWALISHA KUKU WA MAYAI : Kuku wa mayai ili watage vizuri wanatakiwa walishwe chakula bora kwa utaratibu unaotakiwa, ukiwazidishia au kuwaongezea hawatotaga vizuri. Wanatakiwa walishwe kati na kati kulingana na umri kama ifuatavyo:-
Katika umri huu wanapewa chakula aina ya “Super Starter” kwa ajili ya kuwatengenezea kinga mbadala ili waweze kuhimili mikiki mikiki ya vijidudu vya magonjwa kadri wanavyoendelea kukua, wanapewa chakula hicho kwa kiwango maalum kama ifuatavyo:-
Hapa wanakuwa bado ni vifaranga na wanapewa chakula aina ya “Chick Starter” kwa ajili ya kuendelea kuwajenga miili yao waweze kupoekea virutubisho vizuri, hii inatokana na kwamba kuna baadhi ya viinilishe vinafanya kazi ya kumeng’enya chakula na kupatikana viinilishe vingine, kwahiyo vikikosekana katika mwili wa kuku basi hata wale chakula gani bora, hawawezi kutoa mazao bora, lakini kwa kuwapa “Chick Starter” itawapelekea kuwa na virutubisho hivyo muhimu. Kiwango na ulishaji wake ni kama ifuatavyo:-
Katika umri huu kuku wanapewa chakula aina ya “Grower Mash” kwa ajili ya kuwakuza na kuwajenga mfumo wa uzazi kwa maandalizi ya utagaji. Kiwango cha chakula kinategemea na wiki kama ifuatavyo:-
Huu ni umri ambao kuku wanataga kwa kiwango kikubwa sana (85% hadi 100%) hali ambayo inawafanya kutumia nguvu nyingi mno, hivyo hupewa chakula aina ya “Layers Phase 1” kwa ajili ya kufidia nguvu ya ziada wanayotumia ili waendelee kutaga kwa kiwango hichohicho. Ulishaji wake ni kama ifuatavyo:-
Wiki ya 19: Gram 92 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 20: Gram 102 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 21: Gram 108 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 22: Gram 114 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 23: Gram 116 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 24: Gram 120 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 25 – 40: Gram 130 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Katika umri huu kuku wanakuwa wameanza kuchoka na huanza kutaga kwa kiwango cha kawaida (65% hadi 75%) hivyo hupewa chakula aina ya “Layers Phase 2” kwa ajili kuendeleza (maintain) kiwango chao hicho kwa muda mrefu. Kiwango chao ni “Gram 130 kwa kuku mmoja kwa siku moja”.
NB: Kuanzia wiki 81 na kuendelea unaweza kuwauza na kuweka kuku wengine.
0 comments:
Post a Comment