Ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria aina ya haemophilus parragillium 

Jina jingine la infection coryza ni Nobilis coryza

Unashambulia zaidi mfumo wa upumuaji na kusababisha vifo kwa kuku 

Dalili 5 za mafua ya kuku 

1.Kuvimba macho na uso kiujumla (facial swelling)

2.Kukohoa , kupiga chafya mara kwa mara muda mwingine kutoa makamasi (mucuos)

3.Kukosa hamu ya kula na utagaji unapungua kwa kiasi kikubwa kwa kuku wazazi

4.Kupumua kwa shida na wakati mwingine ukoroma 

5.Kubadilika rangi ya upanga na kuwa wa bluu

Kinga

1.Usafi wa banda kila linapochafuka

2.Kutoruhusu watu kuingia hovyo bandani (biosecurity)

3.Kuku mgeni asichanganywe na kuku wengine mpaka muhakikishe hana ugonjwa wowote

4.Hakikisha kuku wako wanapata chanjo , kabla ya kupata ugonjwa

5.Kuku akiwa mgonjwa atengwe mara moja na kuku wazima 

Tiba 

Dawa nzuri ya mafua ya kuku ni FLUBAN, TYLODOX

NB: Ugonjwa wa mafua ya kuku unaanza kuonekana kuanzia  siku 1-3 baada ya kuambukizwa

......................................................................................................................