Kuna
mambo kadhaa ya kuzingatia kabla ya kuchagua aina bora ya kuku wa
kufuga ili ikuletee faida uliyodhamiria. Ufugaji unaweza kukutengenezea
kipato cha ziada au kukupa ajira ya kudumu kama utazingatia yafuatayo.
1. GHARAMA
gharama zitakuongoza kufanya uchaguzi.kuku wa kisasa ni gharama sana.
pia wanahitaji usimamizi wa hali ya juu,lishe kamili na bora ilikuwawezesha kuzalisha
vizuri na kwa ufanisi.kuku wa kienyeji/asili wana gharama ndogo na rahisi kuzoea mazingira ya huku kwetu.
wakipata matunzo bora wanaweza kuboresha uzalishaji.hata hivyo ukitaka kufuga idadi
kubwa na kutumia mlo kamili(balance diet),ni vyema kuchagua kuku chotara(hybrid).
2.HALI HALISI YA SOKO
ni muhimu sana kuzingatia hali halisi au uhitaji wa soko lililokuzunguka.kama soko lipo la kuridhisha
chagua
kuku chotara wenye uzito wa wastani.kama mayai na nyama vinatoka na pia
upatikanaj wa mlo kamili (kuku wa kahawia) ni wa uhakika.
kama unataka kuuza mayai,zingatia jamii ya kuku wepesi (light breed) kuku wale weupe wa mayai.
mazingira mengine tofauti na hapo chagua jamii ya kuku wazito(heavier) mara nyingi wale wa kahawia (brown layers) ndio chaguo linalostahili.
kama unaishi maeneo ya mbali na soko na unataka kuzalisha mayai kwa matumizi ya nyumbani,na kuuza mayai ya ziada
na nyama kwenye eneo ulilopo,hapo chagua kuku wa asili/kienyeji.
3.UZOEFU
kuna msemo unasema "experience is the best teacher" mwalimu mzuri n uzoefu,kama huna uzoefu hata kidogo ni vyema ukaanza
kwa kufuga kuku wa asili ambao ni wa gharama nafuu.
4.USIMAMIZI WA MRADI/BANDA
kama
usimamizi wa banda au mradi wako ni mzuri,anza kufuga kuku wa kisasa
ambao wanafaida kubwa usimamizi mbovu ni sababu mojawapo ya kushindwa
kufanya vizuri kwa miradi mingi na hivyo kupelekea kufungwa.usimamizi
kwenye :usafi,kulisha kiasi sahihi na kwa muda muafaka,kutoa taarifa
haraka,utunzaji kumbukumbu na mengineyo.
5.MAPENDEKEZO YA WENYEJI
inategemea na maeneo,sehemu nyingine hasa mjini,watu hupendelea mayai ya kahawia au yenye kiini cha njano,wengine wanapendelea
mayai ya rangi nyeupe.kumbuka "mteja ni mfalme".
6.UPATIKANAJI WA MBEGU ZA KUKU KIURAHISI
kuku hawa wa kisasa mara nyingi huwa hawapatikani kwa urahisi,inategemea na upatikanaji katika eneo husika.
0 comments:
Post a Comment