script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




Jinsi ya kulisha mbuzi wa maziwa
Jinsi Ya Kuwalisha Mbuzi Wa Maziwa

Ni muhimu kufahamu kuwa chakula unachomlisha mbuzi wako ndicho kitakachotengeneza maziwa hivyo basi ni muhimu:
Kumpa mbuzi chakula katika mahali palipo safi kwa sababu :

o Mbuzi hula kila aina ya chakula hivyo usiwaruhusu kula chakula kilicho na mchanga
o Hali hii huwazuia kuambukizwa minyoo wanaopatikana kwenye mchanga

Mbuzi wa maziwa kwa mara nyingi hufugiwa kwenye zero grazing hivyo basi kumbuka kuwatengezea mahali pa kulia chakula na kunywea maji ambapo panahitajika kuwa juu na mbali na nyumba za kulala ili wasikanyage,au kuchafua chakula

Mbuzi mwenye uzani wa wastani huitaji takriban kilo 500 za chakula cha hali ya juu ama nyasi zilizokaushwa kwa mwaka huku kiwango cha kila siku kikiwa asilimia 5-7 ya uzani wake
Majani kama vile napier, majani ya mahindi au mtama, mboga zisizotumiwa na majani ya viazi yapaswa kukakatwa ili kupunguza uharibifu.

Ondoa chakula ambacho hakijatumiwa kutoka bandani mara mbili kwa siku.ikiwa mbuzi wako hubakisha chakula kingi hii ni ishara ya chakula duni,ama kupewa chakula kingi kupita kiasi,ama mbuzi wako hawana hamu ya kula chakula kwa sababu wana tatizo kama vile kutojihisi vyema

Wape maji safi ya kumywa kwa wingi kama lita 5 kwa kila mbuzi wa maziwa kwa siku
Waweza kuwapa mbuzi nafaka kama njia ya kubadilisha na chakula cha kawaida lakini kumbuka kubadilisha polepole wala si mara moja ili kuwaruhusu mbuzi kuzoea chakula kipya bila kuwadhuru.lakini tahadhari kuwapa mbuzi nafaka tupu kwani saweza kusababisha matatizo ya tumbo
Waweza kuwalisha mbuzi wa maziwa vyakula vya maziwa vinavyolishwa ng’ombe katika kiwango cha nusu kilo kwa mbuzi asiyekamwa,kilo moja kwa mbuzi wa kukama lita moja ya maziwa na nusu kilo kwa kila lita zaidi ya maziwa
Walishe mbuzi madini muhimu kulingana na kiwango cha maziwa wanachotoa

...........................................................................................................................................

0 comments:

 
Top