script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




Kutokana na kuongezeka kwa gharama za chakula cha kuku imewawia vigumu wafugaji wa kuku kupata faida kupitia ufugaji wa kuku.
 Na kwa jinsi utengenezaji wa chakula cha kuku hasa hasa kuku wa kisasa kama broiler na layers kwa wafugaji ni ngumu leo nakuja na somo jepesi la jinsi ya kutengeneza chakula kwa kuku chotara (hybrid) or kuku wa kienyeji wanaofugwa ndani ya banda(Intensive care) kwa kutumia Pearson Square method nahii yote yawezekana kama mkulima atakuwa na raw materials zinazohitajika katika utengenezaji wa chakula.
Njia hii ya pearson square mara nyingi ina base sana katika Digestable crude protein (DCP) ya malighafi husika katika utengenezaji wa chakula. 
Na malighafi zinazotahitajika hapa ni kama vile Mahindi, mashudu ya pamba, mashudu ya alzeti, maharage ya soya na dagaa.

Jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku wa mayai (70kg) (chotara) unahitaji vifuatavyo;

34 kg Mahindi
12 kg Soya beans
8 kg Dagaa
10 kg pumba za mahindi
6 kg Chokaa (kwa ajili ya calcium)

Jinsi ya kutengeneza chakula(70kg) kwa ajili ya kuku wa nyama
Mahindi= 40 kg 
Dagaa = 12 kg 
Maharage ya soya = 14 kg 
Chokaa = 4 kg

NB: Hakikisha unaongeza chumvi 250g katika kila mfuko wa 70kg wa chakula chako

Dondoo muhimu ya jinsi ya kuwalisha kuku wako Nyumbani
· Kuku anaetaga mayai anahitaji kula angalau 130g za chakula kwa siku. 
Kumbuka kuwapa maji masafi muda wote.
· Kifaranga kimoja anahitaji 2.2 kg za chakula kwa wiki 8 (hivyo basi vifaranga 100 = 2.2 kg x 100=220 kg. Vifaranga wanahitaji kula muda wote na pia suala la maji ni muhimu kwao pia na unakumbushwa kuwapa mboga mboga baada ya mlo wao kuisha.
Kuku mdogo anayekaribia kutaga anatakiwa kula 4.5 kg ya chakula kwa muda wa miezi miwili na nusu mpaka watakapoanza kutaga yai kwa mara ya kwanza. Baada ya hapo wanabadilishiwa chakula na kupewa chakula cha utagaji (layer diet). 
· Malighafi zinazotakiwa katika utengenezaji wa chakula zinatakiwa zile za kiwango cha juu kabisa usitumie mahindi yenye uozo maana utafanya kuku wako kupata ugonjwa wa aflatoxins poisoning.
Ukitumia dagaa hakikisha ni wasafi na hawana  shells wa aina yoyote.
· Na mwisho hakikisha chakula hicho unakichanganya vizuri kabisa ili kuleta uwiano au mchanganyo ulio sahihi.

.............................................................................................................................................................

0 comments:

 
Top